Mmanda ametoa agizo hilo katika kikao cha wadau wa Elimu wa halmashauri ya wilaya ya Nanyamba, kufuatia shule ya msingi zaidi ya tano kubainika kuwa baadhi ya wazazi wamewafundisha watoto wao kujaza majibu ya uongo ili wafeli katika mitihani yao.
Kwa upande wa Maafisa Elimu wa msingi na sekondari katika Halmashauri ya Nanyamba, wamesema wamejipanga kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu shule na walimu ili wafanye vizuri kutokana na halmashauri hiyo kuwa nyuma sana kielimu.
Nao wadau wa elimu walioshiriki katika kikao hicho wametoa maoni yao juu ya suala hilo huku wakiitaka serikali kushughulikia kero hiyo pamoja na kuboresha miundombinu ya elimu katika halmashauri hiyo.