Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki, Lucas Mbedule amewaomba msamaha washarika wa Kanisa Kuu la Mtwara ili wasiliumize kanisa.
Amewataka kumaliza tofauti zao na kukutana katika ibada wakiwa na mioyo minyenyekevu kumwomba Mungu.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamekuwa na mgogoro wakimpinga askofu huyo kwa takriban miaka miwili.
Waumini hao wamemwomba Askofu Mkuu wa KKKT, Fredrick Shoo kwenda kuzungumza nao na kuunda tume ya uchunguzi.
Agosti 28,2016 baadhi ya waumini na wazee wa kanisa waliingia katika ibada wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kumpinga askofu huyo kwa tuhuma za kukiuka katiba, unyanyasaji wa watumishi na ubadhirifu wa fedha za usharika na dayosisi.
Umoja wa wazee ulitoa tamko kumwomba mkuu wa kanisa kufanya uchunguzi.
Angalia Video Hii hapa chini>>>>>>>>>>
