"Tulijua tutashinda" – Pole Pole

katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole, amesema chama cha Mapinduzi (CCM) kilijua kuwa kitashinda kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika

Akizungumza na mwandishi wa eatv Polepole amesema watu wameiamini CCM kwa sababu inawajibika kwao, hivyo ahlikuwa suala humu wao kupatra ushindi.
“Niwashukuru kwa kujitokeza, niwashukuru kwa kuwa watulivu, wananchi wengi walionyesha kiu yao ya kupata wawakilishi ambao watwachagua wenyewe, wengi wao walieleza wanapenda kuona kazi nzuri ambayo Rais anaifanya inafanyika katika majimbo hayo, matokeo yameeleza sauti ya watanzania katika maeneo haya, CCM kwa mara nyingine tumeshinda kwa kishindo, sisi tulijua kuwa tutashinda, kwa sababu ya kazi nzuri ambayo serikali ya CCM ilikuwa ikiifanya”, amesema Humprey PolePole.
Licha ya hayo Pole pole amesema kuwa kitendo cha vurugu kilichotokea pia walijua kuwa wapinzani wataleta vurugu, kwani kufanya vurugu ndio kawaida yao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo