Zaidi wananchi 100 wakazi wa kijiji cha Ziwani Kata ya Nyarugusu wamefunga barabara ya kuingilia katika mgodi wa Nyarugusu Mine Co. limited wakishinikiza walipwe fedha zao ikiwa ni fidia ya mazao yao baada ya hekali zipatazo 273 kutiririshiwa maji yenye sumu kutoka katika mgodi huo.
Hatua ya wananchi kufanya hivyo inakuja siku chache baada ya uongozi wa mgodi huo kuandika barua kuwa haitalipa fidia yoyote mpaka pale tathimini ifanyike upya na wananchi wawe na hati miliki ya mashamba yao.
Kufuatia barua hiyo wananchi wameamua kuweka kambi katika barabara hiyo ikiwa ni mita chache kutoka lango kuu la kuingilia mgodini hapo
Diwani wa kata ya nyarugusu Swalehe juma pamoja na Mwenyekiti wa serikali ya kijiji Athuman Selemani wamezungumzia kadhia hiyo.