Mauaji ya Mwanafunzi NIT, Waziri Mwigulu amshukia IGP Sirro

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza mkuu wa jeshi la polisi nchini, IGP Simon Sirro na timu ya uchunguzi kufanya uchunguzi wa kina juu ya kupigwa risasi kwa mwanafunzi Akwilina Akwilini ambaye alikuwa ni mwanachuo wa chuo cha usafirishaji (NIT) yaliyotokea wilaya ya kinondoni  jijini Dar es salaam siku Ijumaa tarehe Februari 18, 2018.

Waziri Nchemba amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo ili kumbaini askari aliyehusika na hilo na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.
Kama Waziri mwenye dhamana nalaani vikali sana tukio la kupoteza maisha ya binti wetu ambaye hakua na hatia, matukio ya namna hii naona yanaanza kujirudia tena kwa kasi matukio ya kupoteza maisha kwa watu wasiokuwa na hatia hasahasa katika masuala yanayohusu siasa ni mambo ambayo hayakubaliki na ninalaani kwa nguvu zote. . Alisema Waziri Mwigulu,“amesema Waziri Nchemba
Ameongeza kwa kusema kuwa amemuelekeza IGP mara baada ya tukio kutokea wafuatilie na wachunguze kubaini wote waliosababisha tukio hilo na kuweza kuwafikisha katika mikono ya sheria ili sheria ichukue mkondo wake.
Dkt. Mwigulu amewataka wananchi wote kuepuka vitendo hivi vinavyoweza kusababisha madhara kwa namna moja au nyingine na wanapoona matukio ya namna hii watoe ushilikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili wausika wafikishwe katika vyombo vya usalama.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo