Wananchi wazuia msafara wa PM, Wamkataa Mkuu wa wilaya

Sakata la Wananchi kuzuia msafara wa Waziri mkuu Kassim Majaliwa, wakiwa na mabango ya kumkataa mkuu wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza Mtemi Msafiri, limechukua sura mpya baada ya Madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kuja juu wakilaani vikali kitendo hicho.
Diwani wa kata ya Ngudu Johanes Malifedha ndiye anayetupiwa lawama na wenzake kwa kuratibu maandamano hayo, ili kupinga maagizo ya mkuu wa wilaya hiyo likiwemo la kupiga marufuku magari yenye uzito mkubwa kutotumia barabara zisizohilimi uwezo wa magari hayo.
Wakizungumza na waandishi wa habari madiwani hao wamelaani kitendo hicho, kutokana na madai kuwa kilio kilichotolewa na Wananchi hao kwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa, kwamba mkuu huyo wa wilaya amekuwa akitoa amri za kuwakamata vijana na kuwatumikisha kwenye mashamba yake hakina ukweli wowote.
Wamesema wanamuunga mkono mkuu wa wilaya ya Kwimba Mtemi Msafiri, kwa kuwa amekuwa akitoa amri kwa vijana wasiopenda kufanya kazi kukamatwa na Jeshi la Polisi, ili waweze kwenda kuwasaidia wazazi wao shughuli za kilimo badala ya kuwatelekeza na kupiga soga vijiweni bila shughuli yoyote.
Channel ikaenda mbali zaidi kutaka kufahamu je, wazazi na wakazi wa wilaya hiyo wanamaoni gani kuhusu msimamo wa mkuu huyo wa wilaya, ambapo wengi wao wameonyesha kufarijika kwa madai kuwa, vijana wengi walitaka kuharibika kutokana na makundi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo