Aliyekuwa diwani wa Kata ya Soitisambu wilayani Ngorongoro mkoania Arusha (Chadema) Boniface Kanjueli amejiuzulu nafasi ya udiwani na kuhami CCM kwa madai ya kupendezwa na utendaji wa rais Magufuli.
Diwani huyu anajiuzulu ikiwa ni siku chache kupita tangu madiwani watatu wa Chadema kujiengua na kuhamia CCM ambao ni Diwani wa Kata ya Ngorongoro, Daniel Orkeriy, Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Wilaya hiyo na pia Diwani wa Kata ya Ngoile, Lazaro Saitoti na Diwani wa Kata ya Loitole, Sokoine Moiv kwa madai ya kuunga mkono utendaji wa rais Magufuli.
