Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo
Wananchi wakifurahia baada ya uzinduzi huo
Muonekano wa zahanati hiyo ya Ilindiwe
Mwenyekiti wa Kijiji akitoa taarifa fupi ya Ujenzi huo
Mganga Mfawidhi Dk Leonard akizungumza na wananchi
Afisa mtendaji kata ya Mang'oto Mengi Chalamila akizungumza kwenye uzinduzi huo
Mgeni Rasmi akitoa hotuba yake
Mganga mfawidhi akimweleza jambo Mgeni Rasmi ndani ya zahanati hiyo
Muonekano wa Mbele wa zahanati hiyo
Hatimaye zahanati ya
kijiji cha Ilindiwe wilayani Makete mkoani Njombe iliyokuwa haijaanza kufanya
kazi kwa miaka 5 baada ya kujengwa, imezinduliwa hii leo tayari kwa kuanza
kuhudumia wananchi wa kijiji hicho
Zahanati hiyo ambayo
kwa kiasi kikubwa imejengwa na wananchi pamoja na mchango wa serikali mpaka
inazinduliwa imegharimu shilingi milioni 52.3
Akisoma taarifa fupi
ya zahanati hiyo mwenyekiti wa Kijiji cha Ilindiwe Bw. Yosofati Idawa amesema
wananchi waliona umuhimu wa kuwa na zahanati hivyo walijitoa usiku na mchana
kuhakikisha inakamilika, huku akizungumzia baadhi ya changamoto wanazokabiliana
nazo ikiwemo kusuasua kutekelezwa kwa ahadi walizoahidiwa wakati wakiendelea na
ujenzi wa zahanati hiyo
Mganga mfawidhi wa
zahanati hiyo Bw. Leonard Mlwilo amewaomba wananchi hao kujiunga mafuko wa afya
ya jamii CHF ambao utasaidia kuimarisha zahanati hiyo hasa kwa upande wa dawa
Diwani wa kata ya
Mang'oto ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa zahanati hiyo
amewashukuru na kuwapongeza wananchi hao kwa michango yao ya hali na mali
iliyofanikisha kukamilika kwa zahanati hiyo
Amesema changamoto ya
rasilimali mbao kama meza na viti wananchi waendelee kujitolea kuhakikisha
vinakuwepo kwa kuwa rasilimali hiyo inapatikana kijijini hapo, huku pia
akiwasisitiza kuweka utaratibu wa kukusanya mchango wa CHF ikibidi uanze mapema
ili manufaa yaende sanjari na kuanza kutumika kwa zahanati hiyo
Kuanza kutumika kwa
zahanati hiyo kutawaondolea kero wananchi wa kijiji hicho ambao walikuwa
wakisafiri umbali mrefu hadi kijiji cha Mang'oto kufuata huduma za kiafya Jambo
lililofurahiwa na wananchi hao










