Mwanafunzi Pekee aliyefeli Makete Kuchunguzwa

Uongozi wa kijiji cha Ilindiwe kwa kushirikiana na wa Kata ya Mang'oto wilayani Makete mkoani Njombe wanafanya uchunguzi wa sababu zilizopelekea mwanafunzi mmoja kufeli mtihani wa kuhitimu darasa la 7 licha ya mwanafunzi huyo kuwa na uwezo wa kielimu darasani
Akizungumza katika mahafali ya darasa la 7  yaliyofanyika leo Novemba 11, 2017 katika shule ya Msingi Ilindiwe, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Faustin Ntakunga amesema katika mtihani wa mwaka huu wamehitimu wanafunzi 6 ambapo kati ya hao mmoja ndiye aliyefeli na kusema wanalazimika kuchunguza kujua sababu za mwanafunzi huyo kufeli ilihali alikuwa na uelewa mkubwa darasani
Mbali na hilo uongozi wa shule hiyo umewakabidhi wanafunzi hao kwa wazazi pamoja na uongozi wa kijiji, ambapo wamepokelewa na Mwenyekiti wa kijiji Bw Yosofati Idawa na Afisa Mtendaji wa Kijiji Victor Mapunda
Akizungumza katika mahafali hayo, Afisa mtendaji wa Kata ya Mang'oto Bw. Mengi Chalamila amewasisitiza wazazi uhakikisha wanafunzi hao wanawapeleka shuleni ili kuepukana na mkono wa sheria endapo hawatafanya hivyo
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafali hayo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mang'oto Mh Osmund Idawa amesema atahakikisha uchunguzi unafanywa kujua sababu za mwanafunzi huyo mmoja kufeli, na endapo itaonekana kulikuwa na shinikizo la mwanafunzi huyo kuambiwa afeli, hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mhusika

Jumla ya wanafunzi 6 wamehitimu elimu ya msingi katika shule hiyo ya Msingi Ilindiwe mwaka huu, huku wanafunzi watano wakifaulu na mmoja kufeli


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo