Rais John Magufuli amempongeza IGP Simon Sirro kwa kupambana na ujambazi na kuwa amefanya vizuri katika hilo lakini bado kwenye suala la watendaji wake wazembe hajafanya vizuri
Rais Magufuli ameyasema hayo leo bandarini jijini DSM wakati akizungumza alipofanya ziara ya kushtukiza na kuangalia magari ya polisi yaliyoingizwa bandarini hapo na kukaa muda mrefu bila kukabidhiwa jeshi la polisi
Amemtaka IGP Sirro kushughulikia uozo kama huo kwa kuwa unamuangusha katika utendaji wake wa kazi