Rais Dkt John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar Es Salaam hii leo na moja ya jambo lililomsikitisha ni kukuta magari ya wagonjwa yaliyoagizwa na mtu asiyejulikana na kuwepo bandarini hapo tangu 2015 bila mwenye nayo kujulikana
Kwa Mujibu wa taarifa zinazotolewa mbele yake sasa hivi na maafisa wa bandari magari hayo yamefika bandarini hapo tangu 2015 Juni na taarifa zikionesha magari hayo yaliagizwa na ofisi ya Rais taarifa ambazo zinaonesha utata
Rais Magufuli amewauliza viongozi mbalimbali lakini bado wameonesha kuyumbishwa kwa kuwa taarifa hizo hazimridhishi
Ametoa siku saba kuanzia leo uchunguzi ufanywe na vyombo vya usalama wamwambie ni mzigo wa nani na hayo magari yameletwa na wakina nani
Pia amechukizwa na mawaziri wa wizara husika kutofahamu kuhusu walioagiza hayo magari
Kwa nini Waziri Hukujua, kwa nini IGP hukujua, kwanini PCCB hukujua, je kwa nini Mimi nijue? amesema Rais Magufuli