Manji Aibwaga Serikali Mahakamani, Aachiwa Huru

Mfanya biashara Yusuf Manji leo Oktoba 6 2017 amefutiwa kesi iliyokuwa ikimkabili ya kutumia dawa za kulevya.


Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kufunga ushahidi.
Sababu ambayo imepelekea kufutwa kwa kesi hiyo imetajwa kuwa ni upande wa mashtaka ambao ni serikali kushindwa kuthibitisha kosa la mtuhumiwa, Yusuf Manji.
Katika kesi hiyo, Manji anadaiwa kati ya Februari 6 na 9, eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine
Mahakama imemuachia huru Manji ikiwa ni siku chache tangu shauri lake jingine la Uhujumu uchumi liondolewe Mahakani hapo na Mkurugenzi wa mashitaka (DPP) ambaye alieleza kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Manji amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga ambapo alijiuzulu wadhifa huo mapema mwaka huu. Pia Manji alikuwa Diwani wa Kata ya Mbagala kabla ya kuvuliwa nafasi hiyo baada ya kupoteza sifa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo