Kiwanda chateketezwa kwa moto

Moto mkubwa umeteketeza kiwanda cha Super doll kilichopo barabara ya Nyerere Dar es Salaam mchana wa leo, na kuteketeza mali za kiwanda hicho

Akiongea, Kamanda wa polisi mkoa wa Temeke, Gilles Muroto, amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, na jeshi la zimamoto linafanya jitihada za kuzima moto huo.
"Ni kweli tuko hapa jeshi la zimamoto linaendelea kuzima moto likishirikiana na jeshi la polisi, na mpaka sasa bado hatujajua chanzo cha moto huu", amesema Kamanda Muroto.
Katika tukio hilo la kuzima moto huo kulijitokeza changamoto kubwa ya magari ya kuzima moto, ambapo kati ya magari 10 ya zimamoto moja ndilo lenye uwezo wa kuzima moto katika kiwanda hicho.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo