Moto ambao mpaka sasa
haujajulikana chanzo chake umeteketeza mashamba ya miti katika Kijiji cha
Lupalilo wilayani Makete mkoani Njombe
Tukio hilo la moto
limeripotiwa kutokea leo majira ya saa sita mchana na mpaka sasa chanzo chake
hakijajulikana huku jitihada za kuuzima moto huo zikiendelea
Tukio hilo ni
muendelezo wa matukio ya moto yanayoendelea kutokea wilayani Makete siku chache
zilizopita ambapo katika kata ya Mbalatse mbali na moto huo kuunguza mashamba
ya miti pia ziliungua nyumba za wananchi
Katika Line ya simu tumezungumza moja kwa moja na Kaimu Afisa mtendaji wa kijiji Cha
Lupalilo ambaye anaelezea hali ilivyo, msikilize hapo chini kwa kubonyeza play:-
