Kiongozi Mwingine wa Upinzani anashikiliwa na Polisi

Polisi nchini Rwanda wamesema wanamshikilia mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara, mama yake pamoja na dada yake



Wiki iliyopita polisi walikuwa wametangaza kuwa mwanasiasa huyo anatuhumiwa kughushi nyaraka wakati alipotaka kuwania urais mapema mwezi uliopita huku familia yake ikituhumiwa kukwepa kulipa kodi.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, polisi wapatao 10 wameingia kwenye makazi anapoishi mwanasiasa huyo na familia yake mtaa wa Kiyovu mjini Kigali na kuruka juu ya lango baada ya kukataliwa kufunguliwa na kumkamata mwanasiasa huyo pamoja na Mama yake na dada yake.
Duru za polisi zimesema kwamba polisi wameamua kwenda kuwakamata baada ya wao kushindwa kuripoti katika idara ya upelelezi ya polisi mara kadhaa.
Wiki iliyopita, polisi wa Rwanda walitangaza kufanya upekuzi katika makazi ya mwanasiasa huyo na kutangaza kwamba ni sehemu ya upelelezi wa mwanzo kuhusu tuhuma za kughushi nyaraka na kukwepa kulipa kodi. Diane Rwigara alikataliwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mwezi wa 8 na baada ye akaanzisha vuguguvu la kukosoa utawala wa nchi hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo