Muuza madawa aiponyoka Jamhuri mahakamani

 Mahakama Kuu ya Moshi imemuachia huru mtuhumiwa wa dawa za kulevya aina ya mirungi baada ya mashahidi upande wa Jamhuri kushindwa kutoa vielelezo vya ushahidi vilivyokamilika.

Mahakama hiyo imeshindwa kutoa hukumu kwa Aizak Mgavao, mkazi wa Same mkoani Kilimanjaro, aliyekamatwa kwa kosa la usafirishaji wa dawa za kulevya  mwaka 2015, na kuachiliwa huru leo Jumatatu.
Akitoa taarifa hiyo Jaji Mfawidhi Kanda ya Moshi, Aishael Sumari amesema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu kutokana na mkanganyiko wa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri hivyo mtuhumiwa hana budi  kuachiliwa huru.
Mgavao alikamatwa Aprili 11 mwaka 2015 katika kituo kikuu cha polisi Moshi akiwa na mirungi kilo 111 yenye thamani ya Sh 5.5 milioni


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo