ABIRIA zaidi ya 1000 waliokuwa wakisafiri na mabasi ya abiria na magari binafsi kutoka Dar es Salaam, Morogoro na mikoa ya kusini nyanda za juu kusini kuelekea Dar es Salaam wamekwama kwa zaidi ya masaa manne baada ya baada ya lori lenye namba za usajili T 720 BLF Scania lililopata ajali kuziba barabara.
Imeelezwa kuwa kukwama kwa abiria hao kulitokana na zoezi la unyanyuaji wa lori hilo lililokuwa limeanguka eneo la milima ya Iyovi Kijiji cha N'gapa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro toka juzi .
Wakizungumzia mtandao wa matukiodaima juu ya usumbufu huo ambao waliupata abiria Deo Sabikwiguna na John Sanga walisema kuwa walikwama eneo hilo toka majira ya saa mbili asubuhi hadi saa 12:58 mchana kufuatia lori lililokuwa likinyanyuliwa kupitia gari maalum za kunyanyua gari zilizoanguka kuweza kuanguka kwa mara ya pili.
" shida iliyopelekea sisi kukaa muda mwingi hapa ni ubishi wa mafundi ambao walikuwa wakivuta lori hilo ila kama wangesikiliza ushauri wa askari wa usalama barabarani aliyekuwa akizuia zoezi hilo kuendelea lori hili lisingeanguka tena na kuharibika zaidi "
Alisema Sanga kuwa askari huyu alizuia zoezi hilo kuendelea baada ya kuwa tayari lori hilo limetolewa kwenye mtaro kusogea barabarani ila mafundi hao walikaidi na kupelekea kutaka kuzipiga na askari huyo kabla ya kuwaacha kuendelea kuvuta na kusababisha lori kuanguka ubavu kwa mara ya pili.
Kwa upande wao mafundi hao waliokuwa wakinyanyua gari hilo walisema kuwa ajali hiyo ilitokea toka juzi na jana wamefika majira ya saa 1:30 asubuhi kuanza shughuli hiyo ila kutokana na eneo lilivyokaa zoezi limeonekana kuwa gumu kutekelezwa kwa urahisi zaidi.
Chanzo: matukiodaima blog
|