TRA Yafunga vituo vyote vya mafuta Wilayani Sengerema Mwanza

Vituo  vyote  vya mafuta ya petroli ,disel na mafuta ya taa wilayani Sengerema, Mwanza vimefungwa kwa muda usiojulikana kwa kushindwa kufunga mashine za kutoa risiti za kielektoniki (EFD) na  kuikosesha serikali mapato.
Kwa mujibu wa tovuti ya MO Blog  imezungumza na Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wilayani Sengerema ili kuthibitisha  suala hili  amedai  yeye hana mamlaka ya kulizungumzia suala hilo  hadi mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole .
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema kuwa wameamua kuvifungia vituo hivyo  kuendelea kutoa huduma kutokana na kutozingatia maelekezo ya serikali ya kulipa kodi kwani vimeonywa kwa muda mrefu bila kutii agizo hilo la serikali.
Kutokana na hali hiyo Kipole amewataka wafanyabiashara kulipa kodi ili kuacha kuibia mapato serikali sambamba na kuwataka wananchi kuacha kulalamika kwani serikali haina lengo la kuwaonea wafanyabiashara.
Kwa upande wao waendesha vyombo vya moto Wilayani Sengerema wamepongeza hatua ya serikali  kuvifunga vituo hivyo vya mafuta licha ya kupata adha ya kukosa huduma hiyo kwa sasa.
Vituo vyote vya mafuta ya petrol, disel na mafuata ya taa wilayani Sengerema vimefungiwa kutoa huduma tangu Julai 14 mwaka huu.
Na Emmanuel Twimanye, Sengerema


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo