Baada ya kuenea kwa taarifa ambazo hazijathibitika katika mitandao ya kijamii kuwa katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA DR Vincent Mashinjiamekamatwa na Polisi akiwa katika ratiba yake ya kuendelea kukagua shughuli za kichama Mbamba Bay.
Dr Mashinji imethibitishwa na msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene kuwa amekamatwa akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Zubeda Sakuru.
Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amesema“Tumepata taarifa kuwa katibu Mkuu amekamatwa dakika kama tano zilizopita tumepata taarifa kuwa katibu Mkuu amekatwa na kawekwa ndani kwa masaa 48”