Jogoo huyo aliwekwa katika baa moja na mganga ili 'kuwanasa’ wezi wiki moja iliyopita. Hata hivyo, hakuna mtu yeyote aliyenaswa, baadhi ya wakazi wakimtaja kama bandia.
Walioiba walitarajiwa “kupata adhabu” yao , ila hakuna lolote liliwafanyikia.
Hapo jana, jogoo huyo alikuwa angali katika mabati ya baa hiyo, ila hakuna tukio lolote ambalo limeshuhudiwa tangu awekwe hapo.
Kwa wiki moja iliyopita, mamia ya wakazi wamekuwa wakifika katika kijiji cha Kagati kumwona jogoo huyo. Baadhi wamekuwa wakitoka mjini Karatina, ulio umbali wa kilomita 20.
Jogoo huyo pia alidaiwa kuwa na nguvu za “kuwafukuza” wezi wanaofika kujaribu kutekeleza wizi katika baa hiyo.
Mmiliki wa baa hiyo aliamua kutafuta usaidizi wa mganga, baada yake kuvamiwa mara kadha.
Mwanakijiji Martin Mwangi alitaja hatua hiyo kama njama ya kuwahadaa.
“Hawa watu wanatudanganya. Hakuna chochote ambacho tumesikia na madhara yake. Huu ni mzaha tu wa kutufunga macho,” akasema. Mmiliki huyo pia hakuwepo.