Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Katibu Mkuu wa Chama Hicho Doyo Hassan katika Maandalizi ya kuazimisha Miaka mitano ya kuzaliwa kwa Chama hicho.
Doyo amesema kuwa Chadema kuingilia Mgororo wa CUF kunaweza kuhatarisha amani ya nchi.
"Tumeshuhudia Migogoro mingi ya vyama vya siasa lakini hatujaona kingene kikiingilia Mgogoro wa Chama kingine".
Hata hivyo Doyo ameitaka serikali iviache vyama vya siasa nchini vifanye shughuli zao.
Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama hicho yatafanyika Tarehe 22 Agosti Mwaka Huu ambapo chama hicho kitakuwa na ziara kwenye asasi za Kiraia, kuwatembea Waginjwa, Wafungwa, Vyuo vikuu na Kutembea Nyerere Foundation ,N.K na Mwisho kuhitimisha kwenye Ofisi za chama hicho Buguruni Jijini Dar es Salaam.