Mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule Profesa Jay leo yupo jimboni kwake mikumia kwa ajili ya kusherehekea ndoa yake na wananchi wa jimbo lake baada ya wiki iliyopita kufunga pigu za maisha katika kanisa la St Joseph jijini Dar es Salaam.
Katika kuonyesha ni namnagani ana mapenzi na wapiga kura wake wa Mikumi leo ameamua kufanya sherehe nyingine baada ya ile ya Mlimani City Dar.
Profesa Jay anafanya sherehe hii ya wazi kwenye uwanja wa Bustani na muda huu kuna gari zima la Cocacola ambalo lipo mahususi kwaajili ya kuwagawia soda wakazi wote wa mikumi waliyojitokeza uwanjani hapa.
Mbali na soda pia Prof Jay amewaandalia chakula cha kutosha ambacho wote watakaotaka kujumuika naye watakula kadri wawezavyo.