Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameonya tabia ya udanganyifu unaofanywa katika elimu hapa nchini kwa kuwa unasababisha kuua elimu badala ya kuiboresha
Rais Magufuli amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa hosteli za kisasa za chuo kikuu cha DSM ambapo amesema ifike mahali TCU iwaache wanafunzi wajichagulie vyuo wenyewe badala ya kupangiwa kwa kuwa hali hiyo inasababisha wanafunzi kupelekwa kwenye vyuo ambavyo havina hadhi
"Kwa kuwa tu serikali itatoa ruzuku kwa vyuo hivyo, basi unakuta hata vyuo visivyo na sifa kulundikiwa wanafunzi wengi, hata kama hawana sifa, hili si sawa na ninajua halitafurahisha wengi, na hapa sipo kumfurahisha kila mmoja" amesema Rais Magufuli
Pia amesikitishwa na kitendo cha mabasi ya chuo kufa, hali inayopelekea wanafunzi kudandia daladala na kupoteza vifaa vyao humo, huku akiuomba uongozi wa chuo hicho kufanya utaratibu wa kununua japo mabasi matano kwa ajili ya chuo hicho
