RAIS Dkt John Magufuli ameshangazwa na kitendo cha mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea kushindwa kwenye tukio la kuzinduliwa kwa hosteli za kisasa za Chuo kikuu cha Dar Es Salaam hii leo
Rais Magufuli amesema ameamua kumuita mbunge huyo kusema au kuomba lolote kutoka kwa Rais na yeye angempatia, lakini kwa kuwa hayupo, wananchi wampelekee shida zao na yeye alizepeke serikalini ili zifanyiwe kazi
Amesema wakati wa kampeni mbunge huyo aliahidi vitu vingi hivyo anatakiwa kushirikiana na serikali kuvitekeleza
Katika hatua nyingine amemsifia katibu mkuu wa wizara ya Maji Prof Kitila Mkumbo na kusema ni mtu safi, na yeye hateui VILAZA
Rais Amesema atamshangaa katibu mkuu huyo endapo chuo kikuu cha DSM kitakosa maji wakati yeye ni mwana jumuia ya chuo kikuu, na pia ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji
Amesema Prof Kitila alipoteuliwa kuwa katibu mkuu, alikwenda ofisi za CCM kutafuta na kuisoma ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya 2015-2020 na kutafuta kipengele cha Maji ili aanze utekelezaji wa ilani hiyo
