Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Edward Lowassa amevunja ukimya na kuzungumzia tukio la kinyama la kuuawa kwa askari polisi 8 wilayani Kibiti mkoani Pwani
Akizungumza mara baada ya kushiriki ibaada ya Pasaka hii leo jijini Dar Es Salaam Lowassa amesema tukio hilo ni baya na halifai kufurahiwa na mtu yeyote na badala yake likemewe na kila mtu
Amesema kitendo cha kuuawa askari polisi hao kimelisononesha taifa, na wananchi wanapaswa kushirikiana na jeshi hilo, na wale wenye taarifa zozote zitakazoweza kulishaidia jeshi la polisi kupata wahalifu waliowaua polisi hao, wakazitoe kwa vyombo husika ili waweze kutiwa mbaroni
Hivi karibuni jeshi la polisi lilipata pigo baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi kuwaua kwa kuwapiga risasi askari polisi 8 wilayani Kibiti mkoani Pwani waliokuwa wakirejea kambini kutoka kwenye majukumu yao ya kila siku ya ulinzi wa taifa
