ASKOFU (mstaafu) wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mdegella amesema watanzania wana mambo mengi ya kufanya ikiwa ni pamoja na kujikita katika shughuli za kiuchumi badala ya kupoteza muda mwingi kujadili mambo ya Daud Bashite.
Akitoa salama za Pasaka jana katika usharika wa kanisa kuu Dkt Mdegella alisema kuwa watanzania wanapoteza muda mwingi kwa jambo hilo badala ya kushughulika na mambo ya msingi yenye tija kwa Taifa .
“ Watanzania wiki tatu tunapoteza muda kwa habari za Bashite na Gwajima …hawa wote wametoka Mwanza wanajuana vizuri nawaombeni watanzania tusipoteze muda bure tujikite kwenye mambo ya kiuchumi mtu kama amedandia vyeti atakamatwa kwa utaratibu sasa sisi tumebaki Bashite Bashite yaani ukitaka kujua nchi hii watu wanapenda majungu angalia walivyokomalia hii la Bashite “
Alisema Dkt Mdegela kuwa watu wanapoteza muda kushinda vijiweni kuzungumia Bashite badala ya kwenda kutafuta shughuli za kiuchumi kwa ajili ya kupata fedha .
Katika hatua nyingine Dkt Mdegella alipongeza kazi nzuri inayofanywa na Dayosisi hiyo chini ya askofu mteule Blaston Gavile kuwa heshima kubwa aliyoionyesha kwa yeye kama askofu aliyeongoza kanisa hilo kwa miaka 30 ya kustaafu imekuwa ni heshima kubwa kwa kanisa hilo ila mrithi wake anafanya kazi aliyomuachia vizuri sana.
Hivyo alishauri kanisa hilo kuanzisha baraza la wazee washauri nay eye atakuwa mwenyekiti wa washauri hao ili kulifanya kanisa hilo kuendelea kufanya mazuri zaidi.
Kwa upande wake askofu Mteule wa Dayosisi ya Iringa katika salam zake aliwataka waumini wa kanisa hilo kuendelea kuuombea mkoa wa Iringa na maeneo mbali mbali kuachana na matukio ya ubakaji na ulawiti ambayo yanazidi kuongezeka siku hadi siku .
“ Salam zangu kwenu waumini ni kuendelea kuomba kwa ajili ya Taifa na mkoa wa Iringa tusema Mungu yatosha kuendelea kusikia matukio ya ajabu ndani ya Taifa letu …tuendelee kuiombea nchi yetu kuwa ni ya amani na kuepuka matukio yote ya utekaji na mauwaji kwenye hili Taifa “
Alisema Kanisa limesikitishwa sana na mauwaji ya askari nane waliouwawa kinyama kwa risasi na kuwa kazi ya wakristo isiwe ya kulalamika mitaani kama ilivyo kwa mataifa kazi kubwa iwe ya kufunga na kuomba kwa ajili ya taifa .