Bashe – Tutakua Tunajenga Taifa la Raia Waoga, Msiingiwe na Woga Juu ya…

LEO Marhi 21, 2017 Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe (CCM)amechapisha ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye maneno haya.
“Kama taifa wazee wetu walipoanzisha harakati za kudai uhuru na hatimaye tukaupata mwaka 1961 walikuwa na malengo
“Upo uwezekano mkubwa kwamba sisi viongozi wa sasa tumewaangusha ninyi raia katika kufikia malengo ya waasisi wetu
Msikubali kuangushwa na sisi wachache, nyinyi ni wengi mna mamlaka na nguvu ya kututaka sisi kuwafikisha kwenye malengo ya Uhuru‘ –Hussein Bashe
Ni jambo la hatari kwa taifa inapotokea viongozi wakakosea na kutoka nje ya malengo, wananchi wakakaa kimya na kuogopa kuonya, kushauri, kukosoa au hata kukemea sababu tu ya woga au hofu.
Tutakua tunajenga taifa la raia waoga msiingiwe na woga juu ya kudai haki zenu na kututaka sisi viongozi kutimiza wajibu wetu
Kwa kushindwa kwenu kutukemea au kutushauri tunapokengeuka sote tunaingia katika kundi moja la kuwakosea na kuwasaliti wazee waliopigania UHURU wa taifa letu. TUJISAHIHISHE‘ –Hussein Bashe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo