Masogange akwama kwenye Foleni wakati Kesi ikiendelea Mahakamani

Upelelezi wa kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Msanii Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) katika Mahakama ya Kisutu bado haujakamilika na imeahirishwa, huku akishindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kukwama kwenye foleni.

Wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliyaeleza hayo leo wakati kesi ilipotajwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri.

Mkini alidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na mshtakiwa hayupo mahakamani hapo.

Baada ya kueleza hayo, wakili wa Masogange, Nictogen Itege ameiarifu Mahakama kuwa mteja wako hiyo alikuwa njiani kuelekea mahakamani lakini alikwama katika foleni eneo la Jangwani.

Kesi imeahirishwa hadi Aprili 20, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo