
Zaidi ya ng’ombe 16,000 wamekufa wilayani Mvomero mkoani Morogoro kutokana na ukame unaoyakabili maeneo mbalimbali hapa nchini.
Katibu wa chama cha wafugaji mkoa wa Morogoro, Kochocho Mgema amewaambia waandishi wa habari kuwa ng’ombe hao wamekufa kutokana na kukosa maji na malisho.
Katibu tawala mkoa wa Morogoro, JOHN NDUNGURU amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wafugaji kupunguza mifugo yao kama walivyoagizwa na serikali kulingana na maeneo yao ya malisho.