Ugeni uliompata Rais Magufuli leo huko Chato

Rais JOHN MAGUFULI amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa NIGERIA Profesa IBRAHIM GAMBARI nyumbani kwake CHATO mkoani GEITA.
Mazungumzo yao yamelenga masuala mbalimbali ya uhusiano kati ya TANZANIA na NIGERIA.
Rais MAGUFULI amempongeza Rais MUHAMMADU BUHARI kwa jitihada anazochukua kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini mwake.
Pia, Rais MAGUFULI amempongeza Rais BUHARI kwa jitihada anazozifanya za kukabiliana na kundi la Boko Haramu ili kuhakikisha amani inaendelea kudumu nchini mwake.
Kwa upande wake Mjumbe Maalum wa Rais wa NIGERIA, Profesa IBRAHIM GAMBARI amempongeza Rais MAGUFULI kwa ushindi alioupata na jitihada anazochukua katika kupambana na rushwa na kubana matumizi jambo ambalo linaungwa mkono na wananchi wengi wa NIGERIA.
Profesa GAMBARI alimkabidhi Rais MAGUFULI barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais MUHAMMADU BUHARI wa NIGERIA.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo