
Kaimu Kamanda wa polisi, wa mkoa wa RUVUMA, DISMAS KISUSI amewataja watoto hao kuwa ni BENJAMIN NDUNGURU mwanafunzi wa darasa la nne na FREDY MATEMBO mwanafunzi wa dasara la kwanza.
KISUSI amesema wanafunzi hao wamepotea tangu Januari sita mwaka huu na miili yao kupatikana Januari nane mwaka huu kufuatia taarifa zilizotolewa na watoto waliokuwa wakiokota maembe kuona miguu imefukiwa na kifusi cha udongo.