Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeuagiza uongozi wa mkoa wa IRINGA kufuata mipaka ya wilaya za KILOLO na IRINGA iliyowekwa kwa mujibu wa gazeti la serikali toleo la mwaka 2002 ikiwa ni jitihada za kusuluhisha mgogoro wa mipaka ya maeneo hayo.
Akizungumza na wakazi wa vijiji vya ILAMBILOLE na ILOLE ambavyo vinapakana kiwilaya, Naibu Waziri wa wizara hiyo ANGELINA MABULA ametoa wiki moja kwa wakuu wa wilaya kukaa na wananchi wa vijiji hivyo ili kumaliza mgogoro huo.