Na Ibrahim Yassin,Rungwe
DIWANI wa kata ya Masebe (CCM) Amani Mwanyingili ameangua kilio kwenye sherehe za kuaga kuitumikia halmashauri katika utawala wao wakiwa madiwani sambamba na kukabidhiwa vyeti huku akiishutumu serikali ya Chama cha Mapinduzi kutompa mradi hata mmoja.
Hayo yalibainika Hivi karibuni mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kuvunja baraza la madiwani ambapo jioni yake ilifanyika tafrija na kukabidhiwa vyeti vya utumishi bora kwenye ukumbi wa DM Hotel Tukuyu mjini na kufikia hatua diwani huyo kumwaga machozi kwa kutopelekewa mradi hata mmoja na kusema wanannchi wanamkejeli.
Katika hafla hiyo diwani waKawetele Nccr Mageuzi na mwenyekiti wa Ukawa aliongoza madiwani wenzake kukabidhiwa vyeti vya uongozi bora zilizoambatana na sherehe zilizojumuisha watendaji,madiwani na kamati ya ulinzi na usalama chini ya mkuu wa wilaya Zainabu Mbusi.
Katika kikao cha kuvunja baraza hilo,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo aliwapongeza madiwani kwa ushirikianao wao katika miaka mitano ambapo alisema wameipa sifa kubwa wilaya hiyo hadi kutunukiwa tuzo ya heshima ya kuongoza kitaifa katika usafi wa mazingira pamoja na kupata hati safi.
Mbusi alisema katika ushirikiano mzuri wa miaka mitano kati ya watendaji na madiwani kuanzia mwaka 2010 wamepata hati safi (Un Qualified Opinion) kwa miaka mine isipokuwa mwaka 2012 walipata hati ya mashaka na kuwa anawaombea katika uchaguzi wa mwaka huu mungu awape nguvu ya ushindi ili wakutane tena.
Mwenyekiti wa halmashauri wilayani humo Mwakipiki Mwakisungura mbali na kupongeza ushirikiano kati yao na watendaji pia kikao hicho kilitumia nusu saa kufanya maombi ya kuwakumbuka madiwani wenzao wawili waliofariki dunia ambao ni Dr,Rhoder Mwaikambo,kata ya Malindo na aliyekuwa mwenyekiti wa halmashuri hiyo John Mwankenja.
Mwenyekiti wa kambi ya upinzani Anyimike Mwasakilali alimueleza mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Zainabu Mbusi kutokuwa na upendeleo katika kufanya kazi za ulinzi kwenye mikutano ya kampeni na kusema kuwa haki itendeke bila upendeleo ambapo muu huyo aliahidi kutend haki.