Askofu Mokiwa azungumza Mambo Mazito, Awataja wanaochochea Mgogoro

Mokiwa.jpg
Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa​



Askofu Mkuu Kanisa la Anglican Dayosisi ya Dar es Salaam, Valentino Mokiwa, amesema migogoro mingi inayotokea katika kanisa hilo ni ya kutengenezwa jambo linalowavunja mioyo waumini.

“Kanisa ndilo kimbilio la waumini wenye shida mbalimbali, sasa kukiwa na migogoro waumini watamkimbilia nani?” alisema

Dk Mokiwa alizungumza hayo jana na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi wa mgogoro ulioibuka hivi karibuni ambapo Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican nchini, Jacob Chimeledya alimtaka Dk Mokiwa ajiuzulu.

Askofu Chimeledya alimtaka Askofu Mokiwa ajiuzulu kwa kile alichodai kuwa anatumia madaraka yake vibaya na ubadhirifu wa fedha.

Hata hivyo, katika kikao chake na wanahabari leo asubuhi, Askofu Mokiwa alikanusha na kudai kuwa migogoro hiyo inapandikizwa na maadui zake.


CHANZO: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo