Akamatwa akiitapeli Serikali ili imsajilie Gazeti Lake

Idara ya Habari (MAELEZO) imebaini nyaraka za kughushi zilizowasilishwa na Mmiliki wa Kampuni ya FUKANI, Joseph Sheka wakati alipoziwasilisha kwa ajili ya kusajili gazeti la LETE MAMBO.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa MAELEZO, Dkt. Hassan Abbasi(pichani juu) amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliwasilisha nyaraka mbalimbali akidai kuwa ni za Mamlaka ya Mapato (TRA) ambazo uchunguzi wa awali umebaini kuwa mihuri na sahihi za baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo zilizotumiwa ni za kughushi.

“Ni vyema jamii ikafahamu kuwa huu siyo wakati wa kujaribu kuishi kwa njia zisizo halali, kila mwananchi anapaswa kufuata taratibu zinatohitajika pindi anapotaka kupatiwa huduma katika maeneo mbalimbali ya ofisi za Umma.

Dkt. Abbasi alitoa rai kwa ofisi mbalimbali za Umma kuwa makini na nyaraka zinazowasilishwa na wateja wao kwani zinaweza kuwa na malengo mbalimbali ya kuiingiza Serikali katika matatizo hivyo kuitia hasara.

Mbali na hayo Dkt abbasi alisisitiza kuwa wale wanaohisi waliwasilisha nyaraka zao na kuona kwamba zina utata kuja kuzirekebisha na watakaobainika kuwa walighushi nyaraka hizo sheria itafuata mkondo wake.

Kwa sasa Idara ya Habari imemkabidhi mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini dar es salaam kwa mahojiano zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo