Mradi wa maji wa sola ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni 7 katika kijiji cha mandaka mnono wilaya ya Moshi umekwama baada ya watu wasiojulikana kuiba Pampu na hivyo kusababisha adha kubwa kwa wananchi wa kijiji hicho kukosa huduma ya maji safi wanamlalamikia mwenyekiti na afisa mtendaji wa kijiji hicho kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo na hivyo kuwataka wajiuzulu nyadhifa zao.
Wamesema kijiji hicho kilipata ufadhili wa mradi huo wa maji ili kuwasasidia wananchi kuondokana na adha ya kutumia maji machafu ambayo yalisababisha wananachi kukumbwa na magonjwa ya milipuko.
Meneja mradi wa maji katika kijiji hicho Bw.Ernest Nduma amesema wanasikitishwa na wizi huo kwa kuwa tangu mradi huo umalizike una muda wa mwezi mmoja sasa.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mandaka Mnono Bw. Hugo Mcharo amesema tayari wanaendelea na uchunguzi kubaini aliohusika na wizi huo pamoja na kumtafuta afisa mtendaji ambaye haonekani kwa zaidi ya miezi miwili.