BAVICHA nao Watoa siku 7 kuhusu Ben Saanane


Dar es Salaam. Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limeeleza kutoridhishwa na jitihada za Serikali za kumtafuta kada wake, Ben Saanane ambaye ametoweka kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi amesema wanashangazwa kuona serikali ikiweka mkazo kumtafuta 'Faru John' badala ya Saanane ambaye ana thamani kuliko mnyama huyo.

"Tunatoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kutoa taarifa itakayowezesha kupatikana kwa Ben. Hilo likishindikana tutakwenda kumuona Rais Magufuli, Ikulu iwe kwa maandamano au utaratibu mwingine," amesema Katambi.

Mwenyekiti huyo amefafanua kwamba Serikali haiwezi kukwepa wajibu wa kumtafuta Saanane kwa sababu ni raia wake na ana haki ya kikatiba ya kupatiwa ulinzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo