Mkazi wa Kitongoji cha Ilongazala, Kijiji cha Businda, Ushirombo wilayani hapa, Sophia Mulimadoke (45) ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga mbele ya watoto wake na watu wasiojulikana.
Tukio hilo ambalo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema linafanyiwa uchunguzi, ambo mawili; imani za kishirikina na kuchelewa kugawa urithi yametajwa kuhusika.
Akisimulia mkasa huo, mtoto wa familia hiyo ambaye hatukuweza kuandika jina lake kutokana na umri alisema walikuja wanaume wawili wakiwa wamevalia makoti marefu meusi nyumbani hapo wakidai wanatafuta ng’ombe wao wawili waliowapoteza.