Ajali yaua Padri na waumini watano


Geita. Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Kanegere, Kata ya Bukandwe, Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Ajali hiyo imetokea  jana saa 9.30 alasiri.

Habari zilizopatikana usiku huu, zinadai kuwa miongoni mwa watu waliofariki ni Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kahama ambaye aliwabeba abiria wanaosemekana ni waumini wa kanisa hilo ambao baadhi yao pia wamefariki dunia.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Salum Ndimu amekiri kupokea maiti wanne na  majeruhi wanane.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo