Mume Asafirisha Maiti ya Mkewe Kwa Mkokoteni

INDIA
MWANAMUME maskini hohe hahe anayeugua ukoma alijaribu kusafirisha mwili wa mke wake aliyefariki kwa mkokoteni, umbali wa maili 90 (kilomita 144) ili amzike kwa heshima.
Ripoti za habari zinasema mwanamume huyo aliyetambulika kama Ramulu alihitaji pauni 60 (Sh7,620) kusafirisha mwili huo kwa ambulensi lakini alikuwa tu na pauni 12 (Sh1,524).
Ilisemekana mke wake, Kavitha, alifariki katika mji wa Hyderabad magharibi mwa India na alitaka kumsafirisha hadi kijijini mwao Medak kwa mazishi ambapo umbali wake ni karibu kutoshana na umbali wa kutoka Nairobi hadi Nakuru ulio kilomita 159.9

Lakini alifanikiwa tu kusukuma mwili huo ukiwa kwa mkokoteni umbali wa maili 37 (kilomita 59.5) pekee kabla kulemewa, akajiangusha chini na kuanza kuomboleza kwa sauti na uchovu mwingi.
“Kutokana na kuwa hakuwa na pesa za kukodisha gari lolote, Ramulu aliweka mwili wa Kavitha kwenye mkokoteni akatembea nao hadi Vikarabad,” msemaji wa polisi alinukuliwa kusema.
Wapitanjia waliamua kumchangia pesa na kugharamia ambulensi ambayo ilimpeleka hadi kijijini mwake.

Imekusanywa na VALENTINE OBARA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo