Imeripotiwa kuwa Bi Fiona Simpson mwenye umri wa miaka 34 na mama wa watoto watatu alipatikana na makosa ya kusababisha vifo vya nyoka hao kwa kutowalisha kwa zaidi ya miezi sita huko Uingereza
Zaidi ya hayo, aliwahifadhi kwenye kisanduku ambacho hakikutiwa joto, hivyo kuwasababishia mahangaiko zaidi.
Kulingana na mashirika ya habari, maafisa wa idara ya utunzaji wa wanyama wa kufugwa nyumbani walipata nyoka hao wakiwa katika hali mbaya, mwingine akiwa na matatizo ya kupumua na akitoa povu mdomoni.
Mama huyo alikiri makosa yake akahukumiwa kutoa huduma kwa jamii kwa miezi 12, mbali na kupigwa marufuku kufuga wanyama.
Ilisemekana alinunua nyoka hao katika mwaka wa 2015 akajifunza jinsi ya kuwatunza kwenye mitandao ya Intaneti, lakini aliacha kuwalisha kwa sababu alikuwa akikumbwa na matatizo ya kiakili kwa sababu ya shida zinazomkumba nyumbani.
Imekusanywa na VALENTINE OBARA