Geofrey Mungai mtoto wa Marehemu amesema marehemu alipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuanza kutapika mfululizo na kudhaniwa kwamba alikuwa amekula kitu kibaya.
Joseph James Mungai alizaliwa tarehe 24 Oktoba 1943
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha amethibitisha kupokea Mungai akiwa bado mjonjwa na kumpeleka katika idara ya wagonjwa mahututi kabla ya kufikwa na mauti saa 11.20 jioni.