Binti wa Chuo Kikuu cha Makumira Adaiwa Kubakwa Hadi Kufa Kisha Mwili Wake Kutupwa

abakwaINASIKITISHA SANA: Binti mmoja ambaye ni model na mwimbaji wa muziki aliyetambulika kwa jina la JULIANA ISAWAFO (pichani) ambaye picha yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia jana ikionesha mwili wake ukiwa umetupwa eneo la Ndoro nje kidogo ya Chuo Kikuu cha Makumira, Arusha baada ya kudaiwa kubakwa na watu wasiojulikana.juliana-1
julianaMmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, (jina lake halikufahamika mara moja) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa ameokotwa majira ya saa tano asubuhi jana akiwa amekufa na mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la mpunga nje kidogo ya eneo la chuo hicho.
screen-shot-2016-11-03-at-7-10-31-amMbali na kuthibitisha kifo hicho, kiongozi huyo ameeleza pia kuwa, msichana huyo ni mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila hakuwa mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai. juliana-2Ameongeza pia kuwa, msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa walimu wa Sanaa chuoni hapo.
juliana-3Mwisho akaeleza hisia zake namna ambavyo familia ya chuo hicho ilivyoguswa na msiba huo kwani msichana huyo alikuwa kama dancer wa matamasha mbalimbali ya Chuo cha Makumira.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo