Nyumba 236 Zaharibiwa na Mvua ya Mawe Chato Mkoani Geita

chato-1CHATO: Nyumba zipatazo 236 katika Kata ya Ilyamchele wilayani Chato zimeezuliwa na mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali usiku wa tarehe 1 Novemba, 2016.
Mvua hiyo pia imeezua jengo la mahabara ya sekondari ya kata ya Ilyamchele, ofisi ya kata na kijiji, Kanisa la AICT Ilyamchele,nyumba ya mwalimu,nyumba ya muuguzi,ghara la pamba na mazao yanayokadiriwa kuwa hekali 113 yameharibiwa vibaya.
chato-2Hakuna vifo ila watu 23 wamejeruhiwa na mmoja amevunjika mguu. Hadi sasa kaya 38 hazina mahali pa kuishi. Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Shaaban Ntarambe tayari amefika eneo la Tukio ambapo amewashukuru wananchi waliojitolea kuwapa hifadhi kaya 38 ambazo nyumba zao zimeharibika kabisa yaani hawana mahali pa kuishi huku akimwagiza mhandisi wa ujenzi kuweka kambi katika eneo hilo ili kuhakikisha miundombinu yote iliyoharibika hasa ile ya umma inarekebishwa mara moja na kuendelea kutoa huduma.lakini pia kawashauri kila kaya kupanda miti kwani kuna ukataji wa miti mkubwa eneo hilo.
Chanzo: Maduka Online


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo