Polisi afikishwa Mahakamani kwa Kupoteza Bunduki

AFISA wa polisi wa kikosi cha Recce mapema Ijumaa alifikishwa mbele ya mahakama ya Nyeri Kenya kushtakiwa na kosa la kupoteza bunduki yake.
Bw Mike Mutwiri Mbuba alishtakiwa kuwa mnamo usiku wa Julai 13-14, 2016 akiwa katika kambi ya mafunzo ya polisi wa Recce iliyo Solio Ranch eneobunge la Kieni, Kaunti ya Nyeri, kinyume na sheria aliacha bunduki yake chini ya godoro jambo ambalo lilisababisha bunduki hiyo kupotea.
Bw Mbuba hata hivyo alikana makosa hayo mbele ya Hakimu Mkazi Onesmus Towet.
Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000 au pesa taslimu Sh40,000.  
Upande wa Mashtaka ulisema wako na polisi saba watakaotoa ushahidi kuhusiana na kisa hicho.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo