Katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano za kubana matumizi kwa maendeleo ya taifa, halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe inakusudia kupunguza siku za vikao vya baraza la madiwani kutoka siku tatu za sasa na kuwa siku mbili
Mapendekezo hayo yanakusudia kuisaidia halmashauri hiyo kupata fedha zitakazoelekezwa kwenye shughuli nyingine za maendeleo ikiwemo kulipa mishahara ya watumishi na mengine ya maendeleo
Akizungumza na Green FM Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bw. Francis Namaumbo amesema wametoa mapendekezo hayo, na kesho wanakusudia kuyapeleka kwenye baraza la madiwani ili waamue kwa pamoja
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa amesema katika kikao kilichofanyika leo kimekuwa na mabadiliko ya uwasilishaji wa taarifa za kata kutoka kwa madiwani ambapo kwa kawaida walitakiwa kila diwani kufika mbele na kusoma taarifa yake, na badala yake taarifa hizo zikawasilishwa kwa kuzikusanya
Amesema ni kweli halmashauri imekusudia kupeleka mapendekezo ya kupunguza siku za kufanya vikao katika baraza la madiwani ili kupunguza gharama za uendeshaji wa vikao hivyo na hii ni kutokana na kuipunguzia mzigo halmashauri hasa katika matumizi ya fedha lakini kazi zote zilizokuwa zifanyike kwa siku hizo tatu kwa sasa zitafanyika kwa siku mbili kama mapendekezo hayo yakiafikiwa na baraza
Baadhi ya madiwani wametoa maoni kuhusu uamuzi huo ambao utajadiliwa kwa kirefu katika baaza la madiwani la kesho

Sikiliza sauti hizi