Waziri
Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CHADEMA jana alitembelea shule ya Nanja iliyoungua moto hivi karibuni
mkoani Arusha.
Akiambatana
na viongozi wengine katika jimbo la Monduli Lowassa aliwataka viongozi
kuhakikisha shule za bweni zinajengwa vizuri na kuwekewa mifumo ya
kujikinga na ajali za moto kama ambavyo sasa shule tano kwa kipindi
kifupi zimeungua moto mkoani Arusha na chanzo kikiwa hakijulikani.
“Napenda
kuwakumbusha wakuu wa shule na viongozi kwamba ni muhimu shule zote za
mabweni ziwezeshwe na zijengwe vizuri huku zikichukuliwa tahadhari zote
za kujikinga na ajali kama hizi, pia nitaungana na uongozi wa jimbo la
Monduli pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha shule hii inarekebishwa
na watoto wanarejea katika mabweni” Alisema Lowassa.
Aidha Lowassa alitumia nafasi hiyo kuwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii kwani elimu ndiyo mkombozi wa maisha yao.