Mbunge aapa kujiuzulu

Mbunge wa Nyando nchini Kenya Jared Okello ametishia kujiuzulu ikiwa kiongozi wa upinzani ( NASA) Raila Odinga hataapishwa kuwa Rais wa wananchi.

Mbunge huyo ambaye anatokea chama cha ODM amesema atachukua hatua hiyo kwa sababu anaamini kuwa mwanasiasa huyo mkongwe ndiye alishinda katika uchaguzi mkuu wa Agosti 8 mwaka huu, lakini akapokonywa ushindi.
Nilienda bungeni si kuwa upande wa upinzani ila kuunga mkono sera za Rais Raila Odinga huku akiendesha majukumu yake kutoka Ikulu. Nimechunguza kwa makini jinsi kura zilivyopigwa mnamo Agosti 8 na kung’amua kuwa Raila alishinda kwa kura nyingi mno, kwa hivyo ikiwa hataapishwa baada ya majuma mawili yajayo, nitajiondoa kuwa mbunge wa Nyando. Siwezi kuketi bungeni na watu waliopanga njama ya kumpokonya Bw Odinga ushindi ili aendelea kukaa kwenye baridi,” amesema mbunge huyo.
Hivi karibuni kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema kwamba lengo lake la kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo liko pale pale, na ataapishwa ili kuwahudumia wananchi waliomchagua, kitendo ambacho kimeanza kupingwa na serikali kwani tayari yupo Rais aliyeapishwa kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Kenya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo