WANANCHI WATAKIWA KUTOA KERO ZAO KWA VIONGOZI WAO NA SI KUWAOGOPA


Mwenyekiti wa chama cha ccm mkoa wa Manyara Lucas Ole Mukusi amewataka wananchi wa kata ya Gallapo mkoani Manyara wahakikishe wanatoa kero zao kwa viongozi wao nasi kuogopa.
Rai hiyo ameitoa wakati akiongea na wananchi wa kata hiyo kwenye ziara yake ya kuwashukuru wananchi kwaajili ya kumchagua kuwa mwenyekiti pamoja na kikazi ya kukagua miradi ya kijamii na kusikiliza kero za wananchi Viongozi hao walioanza kazi kwa Ari mpya na Kazi mpya iliyofanyika kata ya Gallapo mkoani Manyara.

Alisema kuwa mwananchi aliyempigia kura kiongozi kwa hiyari yake mwenyewe anatakiwa kutoogopa kutoa kero yake kwa kiongozi aliyemchagua hivyo asiogope kutoa kero zake alizokuwa nazo.
Pia aliongeza kuwa kiongozi aliyechaguliwa na wananchi anatakiwa kufuata maadili ya uongozi pamoja na kukaa pamoja kuwa na umoja na mshikamano ili kuweza kujenga maendeleo na kusonga mbele.
Alisema kuwa  chama hakiwezi kudumu kama makundi yapo hivyo makundi yanatakiwa kuondolewa na kila kiongozi  wa wilaya,kata  wahakikishe wanawasikiliza kero za wananchi  iliwasiweze kufarakana bali waweze  kuenzi mambo yaliyoachwa na hayati baba Juliasi Nyerere.

‘’viongozi nawaomba kuwa ninyi ndio viongozi mliochaguliwa mnatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuleta maendeleo kwa wananchi wenu nasi kuwakatisha tamaa pia mnatakiwa kusikiliza kero zao na kuwasomea taarifa za maendeleo ili waweze kujua kinachoendelea.Alisisitiza mwenyekiti Ole Mukusi.

Alisema kuwa viongozi wote wa chama  jukumu lake ni kusimamia kwa uaminifu ili kuleta maendeleoya Tanzania hawataonewa haya au kuvumiliwa akienda kinyume cha hapo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo