Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa wanawake wanaojiuza miili yao
Zanzibar maarufu kama madada poa yameongezeka kutoka asilimia 10 hadi19
hali ambayo inaonyesha kuwa Ukimwi bado ni tishio.
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Abdulhabib Fereji alisema
kiwango cha maambukizi ya Ukimwi Zanzibar kimefikia asilimia moja kutoka
asimilia 0.6.
Alisema maambukizi yapo juu zaidi hasa katika makundi maalum likiwemo
la wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na kuwa maambukizi hayo
kwa mwaka 2007 yalikua asilimia12 hadi kufikia asilimia 2.6 mwaka 2012.
Alisema kwa vijana wanaotumia dawa za kulevya,maambukizi yalikua
asilimia 16 hadi asilimia 11.3 na alisema yanaongezeka kutokana na
Zanzibar imezungukwa na mazingira hatarishi na kuwa mabadiliko ya haraka
ya tabia za kufanya maamuzi sahihi ndani ya jamii katika kukabiliana na
maambukizi mapya.